Kelvin Kimani

ULIPO

Shairi

Ningalijua ningalisema,

Ila mtima ulilegea,

Utambuzi ukakosa,

Na hekima ukatupa.

Muda n’kapoteza,

Bughudha zikajaa,

Madonda sugu ‘kanitesa,

‘Kaniacha mimi hoi,

Sijiwezi, sijifai, sikufai.

Mola pia ‘kafunga tariki,

Dua zikawa hazifiki.

Ila fadhila n’meomba,

Kiapo nimesema.

N’tajikokota, n’jivute, n’kusake,

N’kimbie ulipo,

N’kwame ulipo,

N’lie, n’cheke, nife ulipo.

Curious about something? Wanna Leave a Message?